Ulimwengu
1 dk kusoma
Trump kukifanya Kiingereza lugha rasmi nchini Marekani
Kati ya majimbo 50 nchini Marekani, ni majimbo 32 tu ambayo yamepitisha Kiingereza kama lugha yao rasmi, kulingana na ‘ProEnglish’, taasisi yenye kuunga matumizi lugha ya hiyo.
Trump kukifanya Kiingereza lugha rasmi nchini Marekani
Kiongozi huyo kutoka chama cha Republican ameonesha msimamo wake dhidi ya wahamiaji haramu nchini humo, ikiwa ni pamoja na kukuza matumizi ya lugha ya Kiingereza kwenye hadhara.
tokea masaa 5

Rais Donald Trump anatarajiwa kutia saini amri ya kukifanya Kiingereza kuwa lugha rasmi ya mazungumzo nchini Marekani.

Nchi hiyo haijawahi kuwa na lugha rasmi japo baadhi ya majimbo nchini humo yanakichukulia Kiingereza kama lugha rasmi.

Kati ya majimbo 50 nchini Marekani, ni majimbo 32 tu ambayo yamepitisha Kiingereza kama lugha yao rasmi, kulingana na ‘ProEnglish’, taasisi yenye kuunga matumizi lugha ya hiyo.

Kiongozi huyo kutoka chama cha Republican ameonesha msimamo wake dhidi ya wahamiaji haramu nchini humo, ikiwa ni pamoja na kukuza matumizi ya lugha ya Kiingereza kwenye umma wa watu.

Hata hivyo, suala la lugha ya Kiingereza nchini Marekani bado limezua ‘sintofahamu’, ambapo majimbo kadhaa likiwemo Texas, wanatumia lugha ya kihispania katika matumizi yao ya kila siku.

Mwaka 2011, seneta wa Jimbo la Texas alimuamuru mwanaharakati mmoja wa wahamiaji kuzungumza kwa lugha ya Kiingireza na sio Kihispania.

Suala hilo pia limekumbushia mijadala ya nyuma, ya iwapo ilikuwa ni sawa kwa kutumia lugha ya Kihispania katika eneo la Texas, ambalo hapo awali ilikuwa sehemu ya nchi ya Mexico.

Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us