Mazingira
2 dk kusoma
Takriban watu 30 wapoteza maisha katika maporomoko ya ardhi nchini Uganda
Maafisa wa serikali nchini Uganda wanasema maafa hayo yamesababisha vifo vya takriban watu 30 na kuharibu makazi ya watu mashariki mwa nchi.
Takriban watu 30 wapoteza maisha katika maporomoko ya ardhi nchini Uganda
Maporomoko katika wilaya ya Bulambuli Mashariki mwa Uganda
27 Februari 2025

Kufuatia mvua kubwa iliyonyesha Novemba 27, 2024, maporomoko ya ardhi yaliikumba wilaya ya Bulambuli, mashariki mwa nchi.

Vijiji vilivyoathiriwa ni pamoja na Masubu, Nameche Trading Centre, Mamono, Tangalu, Buzemulili, Masoola katika Kitongoji cha Buluganya, Wilaya ya Bulambuli.

Takriban watu 30 wamefariki baada ya maporomoko ya ardhi katika kijiji kimoja mashariki mwa Uganda, amesema afisa wa eneo hilo siku ya Alhamisi, akionya kwamba huenda idadi hiyo ikaongezeka.

"Tumepoteza takriban watu 30," Mkuu wa Wilaya ya Bulambuli, Faheera Mpalanyi, aliiambia AFP baada ya maporomoko ya ardhi kupiga kijiji cha Masugu, na kuongeza kuwa miili sita, ikiwemo ya mtoto mchanga, imepatikana.

"Kutokana na uharibifu na ukubwa wa eneo lililoathiriwa na jinsi familia zilizoathiriwa zinatuambia, watu kadhaa wamepotea na pengine wamefukiwa kwenye vifusi," alisema.

Tukio hilo liliacha kaya 40 zikiwa zimezikwa kabisa, huku nyengine zikiharibiwa kiasi, kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uganda.

Kufikia sasa, miili 13 imepatikana na timu ya Chama cha Msalaba Mwekundu cha Uganda (URCS), ikifanya kazi kwa ushirikiano na mamlaka za mitaa na wanajamii.

Ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda imesema takriban nyumba 20 zinahofiwa kusombwa na maji.

Awali, tahadhari ya kutokea kwa maafa ilitolewa kupitia mtandao wa X: "Mvua kubwa iliyonyesha Jumatano katika maeneo ya Uganda imesababisha hali ya maafa katika maeneo mengi."

Taifa hilo la Afrika Mashariki limekumbwa na mvua kubwa katika siku za hivi majuzi, huku kukiwa na mafuriko kaskazini-magharibi baada ya mkondo wa mto Nile kuvunja kingo zake na kusababisha timu za dharura kuhangaika kuwaokoa madereva waliokwama.



Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us