Sekta ya anga Afrika kuingiza faida ya Dola Milioni 200 ifikapo 2025
Licha ya faida hiyo, sekta ya usafiri wa anga barani Afrika bado inakabiliwa na gharama za kubwa za usafiri.
Sekta ya anga Afrika kuingiza faida ya Dola Milioni 200 ifikapo 2025
Utabiri wa IATA unaonesha kuwa sekta ya usafiri wa anga barani Afrika, itaingiza faida ya dola 1 kwa kila abiriam kutoka kiasi cha awali cha dola 0.9 kwa mwaka 2024, wakati mahitaji ya mapato kwa mwaka 2025, yanatarajiwa kufikia asilimia 8./Picha: KenyaAirways
27 Februari 2025

Sekta ya anga barani Afrika inatarajiwa kuingiza faida ya Dola za Kimarekani 200, ifikapo mwaka 2025.

Kulingana na shirika la kimataifa la usafiri wa anga (IATA), kiasi hicho ni ongezeko la Dola Bilioni 0.1, kwa mwaka 2024.

Utabiri wa IATA unaonesha kuwa sekta ya usafiri wa anga barani Afrika, itaingiza faida ya dola 1 kwa kila abiriam kutoka kiasi cha awali cha dola 0.9 kwa mwaka 2024, wakati mahitaji ya mapato kwa mwaka 2025, yanatarajiwa kufikia asilimia 8.

Hata hivyo, bara la Afrika bado linaongoza kwa kuwa na gharama za juu za usafiri wa anga kutoka nchi moja kwenda nyingine, huku tatizo kubwa likiwa ni uchache wa sarafu ya dola za kimarekani katika baadhi ya nchi pamoja na mifumo dhaifu ya uunganishaji ndege.

“Tunategemea kuona mashirika ya ndege barani Afrika yakiingiza faida ya dola bilioni 36.6 ifikapo mwaka 2025,” alisema Willie Walsh, Mkurugenzi Mkuu wa IATA.




Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us