Kiongozi wa kikundi cha PKK Abdullah Ocalan ametoa wito wa kuvunjwa wa makundi yote yaliyo chini ya taasisi hiyo na kutaka kusitishwa kwa vitendo vya kigaidi vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 40.
Katika barua yake aliyoandika akiwa jela, Ocalan alisema: Makundi yote yaweke silaha chini, na PKK livunjwe."
Kiongozi huyo aliye kifungoni alieleza "wito huo ulitolewa na Devlet Bahceli, pamoja na Rais Recep Tayyip Erdogan, na majibu chanya kutoka kwa vyama mbalimbali vya kisiasa yanatoa wigo wa kuweka silaha chini."
“...Ni lazima vikundi vyote viweke silaha zao chini kundi la PKK livunjwe."
Licha ya Makamu Mwenyekiti wa chama tawala nchini Uturuki cha AK Efkan Ala, kupokea taarifa hiyo, bado aliweka msisitizo wa kusubiri kwa hatua stahiki zaidi.
“Tutaangalia matokeo yake,” alisema Ala alipoulizwa kuhusu wito wa Ocalan. Kulingana na Ala, iwapo PKK itazingatia wito huo, basi Uturuki itakuwa “huru kutoka kwenye minyororo yake.”
Kikundi cha PKK, kinajulikana kama kikundi cha kigaidi na mataifa mbalimbali ikiwemo Uturuki, Marekani na Umoja wa Ulaya, kikiwa kimesababisha vifo vya zaidi ya watu 40,000 wakiwemo watoto, akina mama na wazee.
Pata habari zaidi kupitia Whatsapp channels