Afrika yazalisha tende zaidi duniani
Afrika
2 dk kusoma
Afrika yazalisha tende zaidi dunianiAfrika inazalisha kiwango kikubwa zaidi cha tende duniani? Naam, Misri inafahamika kwa uzalisahaji mkubwa wa tende duniani huku ikivuna takriban tani milioni 1.8 kwa mwaka.
date palm trees / tende
27 Februari 2025

Na Coletta Wanjohi

Msimu wa ulaji tende kwa wingi umewadia huku siku chache zijazo Waislamu wakianza kufunga kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Wengi wetu hudhania kuwa tende nyingi hutoka katika mataifa ya uarabuni tu, lakini unajua kuwa Afrika inazalisha kiwango kikubwa zaidi cha tende duniani?


Naam, Misri inafahamika kwa uzalisahaji mkubwa wa tende duniani huku ikivuna takriban tani milioni 1.8 kwa mwaka.Nchi zingine barani Afrika ni pamoja na Algeria, Sudan , Tunisia , Libya, Morocco, Mauritania , Chad ,Somalia na Niger . 

Kuzalisha tende kunahitaji subira. Kwa kawaida msimu wa kupanda ni kati ya Februari na Machi .


Awamu ya kutoa maua huanza kutoka kwa mmea baada ya kati ya miaka 4 hadi 8 ya kupanda mbegu ya tende.

Jua na mchanga wenye rotuba ni muhimu kwa zao hilo. Tende huanza kuonekana mtini kati ya miaka 5 na 8 baada ya maua kuchanua kwenye mti huku kukiwa na mafungu ya tende .

Hapo sasa unafahamu kuwa kuvuna hakuko mbali.

Mti wa tende huchukua kati ya miaka 8 na 12 kukomaa kabisa.
Mitende inaweza kuwepo kwa zaidi ya miaka 100, lakini uzalishaji wao unaweza kuwa kati ya ya miaka 30 na 50.


 Msimu wa kuvuna huwa kati ya mwezi wa Septemba na Disemba . Mtende unaweza fika urefu wa zaidi ya mita 36.

Tende zinabadilika rangi kutoka njano, hadi kahawia na baada ya kukauka huwa kahawia iliyokolea.
Wakulima hupanda juu ya mitende mirefu kwa kutumia ngazi aina tofauti ili kuzikusanya, kwa kawaida mchana ili kuepuka joto kali zaidi.


Tende inaweza kuvunwa ikiwa kavu. Tende zilizokaushwa huachwa kwenye jua kabla ya kuwekwa kwenye vikapu . Baada ya hapo zitapelekwa viwandani kwa ajili ya kuwekwa vizuri ndani ya mifuko au vifaa vingine vya kuhifadhia.


Baada ya kuvunwa tende nyingi hukaushwa. Zingine huuzwa zikiwa nzima huku zingine zikichakatwa zaidi kwa ajili ya kutumiwa katika vyakula tofauti.


Tende inaweza kutengeneza maji ya sharubati au juisi, jam na wakati wa Ramadhan ni utaratibu muhimu kwa Waislamu kufungua saumu zao kwa tende.


Ina manufaa kwa mwili ikiwa na madini kama potasiamu na magnesi.


Wataalam wanasema soko la tende linakuwa kwa kasi sana kutokana na uasili wake kupata umaarufu hasa kwa kuwa ina ladha bora na  virutubisho muhimu kwa mwili..

Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us