Afrika
2 dk kusoma
Zaidi ya watu 8,500 wameuawa DRC tangu Januari 2025
Waziri wa Afya wa DRC Samuel-Roger Kamba anasema kuwa zaidi ya watu 5,700 pia wamejeruhiwa katika mashambulizi ya M23 mashariki mwa DRC
Zaidi ya watu 8,500 wameuawa DRC tangu Januari 2025
Kijana mwenye umri wa miaka 27 alijeruhiwa alipokuwa akihudhuria mkutano huko Bukavu, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mnamo Februari 27, 2025. REUTERS/Crispin Kyalangalilwa
tokea masaa 9

Idadi ya watu waliouawa huko Goma na maeneo ya karibu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) imezidi 8,500 tangu Januari, wakati waasi wa M23 walipozidisha mapigano na vikosi vya serikali na kuuteka mji huo, mamlaka zilisema.

Waziri wa Afya Samuel-Roger Kamba alisema Alhamisi kuwa kuna zaidi ya majeruhi 5,700.

"Tayari tumezika zaidi ya watu 8,500 katika mji wa Goma. Bado tuna takriban miili 30 katika vyumba vyetu vya kuhifadhia maiti," Kamba aliwaambia waandishi wa habari katika mkutano wa kutathmini hali ya mgogoro huo kwa sasa pamoja na matatizo ya rais huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.

"Katika siku mbili zilizopita pekee, tuliokota miili 23 ya watu waliouawa kati ya Februari 23 na 25."

Kamba alisema serikali pia ililaani kulazimishwa kwa vijana kujiunga na wapiganaji wa waasi, akibainisha kuwa "malori manne hadi sasa yamewachukua vijana ili kuwalazimisha kujiunga na maadui zetu."

Vifo 1,500 zaidi

Mapema wikihii, Waziri Mkuu alisema takriban watu 7,000 wameuawa tangu Januari, ambayo ni sawa na ongezeko la 1,500 la vifo.

Mnamo Januari 27, waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, walidai kutwaa Goma, huku serikali yenye ambayo makao makuu yake ni mjini Kinshasa ikidai kuwa majeshi ya Rwanda yalikuwepo katika mji huo.

Siku ya Alhamisi, mabomu mawili yalilipuka kwenye mkutano wa waasi wa M23 huko Bukavu, mji mwingine uliodhibitiwa na kundi hilo mashariki mwa DRC, na kuua takriban watu 11 na kuwajeruhi wengine 65.

Kundi la M23 linasema kuwa linatetea maslahi ya Watutsi wachache nchini DRC, ambao wanasema wanabaguliwa kutokana na uhusiano wao wa kikabila na jamii ya Watutsi wa Rwanda.

Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us