Afrika
4 dk kusoma
Mustakabali wa Afrika unategemea maono, utekelezaji, na ujasiriamali
Maono bila utekelezaji ni ndoto ya mchana. Mara nyingi, Afrika imekuwa nyuma si kwa ukosefu wa mawazo mazuri, lakini kwa utekelezaji dhaifu.
Mustakabali wa Afrika unategemea maono, utekelezaji, na ujasiriamali
Wavumbuzi wa Kiafrika wanatatua matatizo ya ndani yenye athari za kimataifa, kutoka kwa benki mtandaoni hadi kilimo kinachoendeshwa na teknolojia. /Picha: IE Network Solutions
27 Februari 2025

Na Meried Bekele

Bara la Afrika lipo kwenye njia panda. Likiwa na idadi kubwa ya vijana, maliasili kubwa, na ulimwengu unaozidi kushikamana, bara hili lina uwezo wa kufafanua upya nafasi yake katika uchumi wa dunia. Walakini, uwezo pekee hautoshi.

Tofauti kati ya kutokua mabadiliko na kuwepo kwa mabadiliko iko katika nguzo tatu muhimu: maono, utekelezaji, na ujasiriamali.

Katika kitabu changu, 'Ethiopia Incorporated', ninachunguza jinsi nguzo hizi zimesaidia safari ya kiuchumi ya Ethiopia na jinsi vinaweza kutumika kwa upana zaidi barani Afrika.

Lakini huu sio tu mjadala, nimeshuhudia wakati nikiunda Mitandao ya 'IE' kuwa mojawapo ya kampuni kuu za teknolojia ya habnchini Ethiopia.

Ilianzishwa mwaka wa 2008, 'IE Networks' sasa ina wafanyakazi zaidi ya 200 walioidhinishwa na imeshirikiana na chapa kuu za kimataifa na watoa huduma mashuhuri wa Ethiopia.

Safari yangu kama mjasiriamali imeimarisha imani yangu kwamba mustakabali wa Afrika utajengwa na wale wanye ujasiri kuwazia jambo kubwa zaidi, kutekeleza bila kuchoka, na kukumbatia uvumbuzi.

Maono ya siku za mbele

Nchi, au biashara, bila maono hudidimia, ikikabiliana na misukosuko badala ya kujenga mustakbali yake yenyewe. Nia yangu haikuwa tu kuanzisha biashara nyingine ya IT, lakini kuunda kampuni ambayo ingeendesha mabadiliko ya kidijitali nchini Ethiopia na kwingineko.

Hadithi nyingi za mafanikio za kiuchumi barani Afrika, iwe katika sekta ya viwanda nchini Ethiopia, mageuzi ya kidijitali ya Rwanda, au kuimarika kwa teknolojia ya kifinolojia ya Nigeria, zilianza kwa maono ya ujasiri.

Viongozi, serikalini na wafanyabiashara, lazima waeleze wazi mikakati ya muda mrefu inayovuka mizunguko ya kisiasa na masilahi ya kibinafsi.

Kuziba pengo kati ya mawazo na utekelezaji

Maono bila utekelezaji ni ndoto ya mchana. Mara nyingi, Afrika imekuwa nyuma si kwa ukosefu wa mawazo mazuri, lakini kwa utekelezaji dhaifu.

Tunapojitosa katika mfumo ikolojia wa teknolojia, tunahitaji kukumbuka kuwa maono thabiti peke yake hayatoshi, tunahitaji kuunda timu inayofaa, kuanzisha nidhamu ya utendaji kazi, na kuangazia changamoto za kufanya biashara katika soko linaloendelea.

Ubia wenye mustakabali hufeli kwa sababu wanapuuza umuhimu wa utekelezaji.

Nchi ambazo zimepata maendeleo, kama Mauritius au Botswana, zimefanya hivyo kwa kuhakikisha kwamba taasisi, sera na vivutio vinalingana na malengo yao ya muda mrefu.

Utekelezaji unahitaji nidhamu, uwajibikaji, na uwezo wa kujifunza kutokana na vikwazo.

Kuendesha uvumbuzi na ukuaji

Nguzo ya mwisho ni ujasiriamali, injini ya mabadiliko ya kiuchumi.

Kote barani Afrika, wabunifu wachanga wanatatua matatizo ya ndani yenye athari za kimataifa, kutoka kwa benk mtandaoni hadi kilimo teknolojia.

Lakini ili ujasiriamali ustawi, ni lazima uungwe mkono na sera zinazopunguza vikwazo vya urasimu, kuboresha upatikanaji wa mtaji, na kuunda mazingira ambapo ujasiri hutuzwa.

Serikali, wawekezaji, na taasisi za elimu zote zina jukumu la kutekeleza katika kukuza utamaduni ambapo uundaji wa biashara unaonekana kama kipaumbele cha kitaifa.

Nilipoanzisha biashara yangu, nilijua kuwa soko halikuhudumiwa vizuri, lakini pia nilijua kwamba mafanikio yangehitaji zaidi ya kutambua fursa, itadai uthabiti, fikra za kimkakati, na kubadilika.

Leo, mafanikio yetu ni uthibitisho kwamba wafanyabiashara wa Kiafrika wanaweza kujenga makampuni ya kiwango cha kimataifa, hata katika mazingira yenye changamoto.

Mtazamo kama huo lazima uendelezwe katika bara zima. Nguvu kazi ya kimataifa. Moja ya raslimali kubwa ya Afrika ambayo haijatumiwa ni vijana wake.

Kwa umri wa wastani wa miaka 19 tu, idadi ya vijana wa bara ni nguvu ya kiuchumi inayosubiri kufanyiwa kazi.

Vipaji viliopo barani Afrika sio tu maliasli ya ndani, ni fursa ya kimataifa.

Kuanzia wahandisi wa programu nchini Kenya hadi wabunifu wa kidijitali nchini Ghana, vijana wa Kiafrika tayari wanathibitisha uwezo wao wa kushindana katika nafasi kubwa duniani.

Walakini, kwa vijana wa Kiafrika kutumika kama nguvu kazi ya kimataifa, uwekezaji katika elimu, miundombinu ya dijiti ni muhimu.

Ulimwengu unapitia mabadiliko kuelekea kazi za kampuni moja zinazofanywa sehemu tofauti au hata nyumbani, na Afrika ina uwezo wa kuwa katikati ya mageuzi haya.

Kwa mafunzo sahihi na muunganisho, mamilioni ya vijana wa Kiafrika wanaweza kushiriki katika uchumi wa dunia, sio kama watumiaji, bali kama wabunifu na watoa huduma.

Mafanikio ya mfano wa Ethiopia, kama sehemu kubwa ya Afrika, bado inaandikwa. Nchi imepiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi, lakini bado kuna changamoto.

Kwa kukumbatia maono, utekelezaji, na ujasiriamali, Ethiopia na Afrika kwa ujumla inaweza kuunda njia kuelekea ustawi endelevu. Wakati wa kuchukua hatua ni sasa.

Mustakabali wa Afrika hautaamuliwa na nguvu za nje pekee, bali kwa ujasiri wa wenye maono yake, nidhamu ya watekelezaji wake, na werevu wa wajasiriamali wake.

Muhimu zaidi, itaendeshwa na nguvu na talanta ya vijana wake, ikiwa itapewa fursa sahihi za kustawi.

Mwandishi: Meried Bekele, ni mwandishi, mjasiriamali, na mbunifu wa mtandao.

Maoni yaliyotolewa na mwandishi hayaakisi maoni na sera za uhariri za TRT Afrika.

Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us