Afrika
2 dk kusoma
DRC yafanya uchunguzi wa ugonjwa usiojulikana
Mlipuko wa hivi majuzi ulitokea katika kituo cha afya cha Basankusu, ambapo wiki iliyopita watu wengine 141 waliugua, ingawa hakuna vifo vilivyoripotiwa.
DRC yafanya uchunguzi wa ugonjwa usiojulikana
Daktari kwa akina mama wa DRC katika hospitali inayosimamiwa na Medecins Sans Frontieres (MSF) huko Bunia, kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Juni 27, 2003.
tokea masaa 8

Mamlaka ya afya katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wataalamu kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) wanafanya uchunguzi zaidi kubaini chanzo cha aina nyingine ya ugonjwa na vifo vya watu kadhaa katika mkoa wa Equateur.

“ Katika miezi ya hivi karibuni, ufuatiliaji wa magonjwa umebainisha ongezeko la magonjwa na vifo mara tatu zaidi katika maeneo tofauti ya nchi, na kusababisha uchunguzi ili kuthibitisha dalili na kutoa msaada unaohitajika,” WHO imesema katika taarifa.

Tangu mwanzoni mwa 2025, mkoa wa Equater umeathirika kwa magonjwa na watu kufariki kutoka na magonjwa.

Mlipuko wa hivi majuzi ulitokea katika kituo cha afya cha Basankusu, ambapo wiki iliyopita watu wengine 141 waliugua, ingawa hakuna kifo chochote kilichoripotiwa.

Katika eneo hilo hilo, kumekuwa na maambukizi 158 na vifo 58 katika kituo kimoja cha afya mapema mwezi wa Februari.

Mnamo Januari, kituo cha afya cha Bolamba kiliripoti kuugua kwa watu 12 ambao na vifo vya watu 8.

Changamoto ya magonjwa

“ Uchunguzi umebainisha kuwa jumla ya wagonjwa 1096 na vifo 60 katika maeneo ya Basankusu na Bolomba yanayolingana kwa dalili kama vile homa, maumivu ya kichwa, baridi, jasho, kukamaa kwa shingo, maumivu ya misuli, maumivu mengi ya viungo na mwili, kutokwa na damu puani, kikohozi, kutapika na kuhara,” WHO imeongeza.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inakabiliwa na migogoro mingi na milipuko ya magonjwa, na hivyo basi kuongeza mzigo kwa sekta ya afya pamoja na watu.

Katika kukabiliana na mlipuko wa hivi punde wa ugonjwa, maafisa wa kitaifa wametumwa kutoka Kinshasa na Equateur ikiwa ni pamoja na wataalamu wa kukabiliana na hali ya dharura wa WHO katika vituo vya afya vya Basankusu na Bolomba kuchunguza hali hiyo na kubaini kama kuna msururu wa matukio usio wa kawaida.

Miongoni mwa majukumu yao wataalamu hao wanafuatilia mienendo ya magonjwa, kufanya mahojiano na wakazi ili kufahamu historia, na kutoa matibabu ya magonjwa kama vile malaria, homa ya matumbo na uti wa mgongo.


Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us