Kwa nini nchi za Kiafrika zinaikataa Ufaransa, na kuikumbatia Uturuki?
Siasa
4 dk kusoma
Kwa nini nchi za Kiafrika zinaikataa Ufaransa, na kuikumbatia Uturuki?Kupanuka kwa pengo la Ufaransa Afrika Magharibi na Kati na kuzibwa na mataifa mengine yenye nguvu kama Uturuki, ambayo yanafuata mkondo tofauti katika uhusiano na mataifa ya Afrika.
Kutoka kushoto: Viongozi wa Burkina Faso, Mali, Senegal na Chad ni miongoni mwa waliokomesha ushirikiano wa kijeshi na mkoloni wa zamani Ufaransa.
27 Februari 2025

Na Emmanuel Onyango & Susan Mwongeli

Enzi za utawala wa Ufaransa katika makoloni yake ya zamani barani Afrika zinaonekana kuisha, kwani Paris inazidi kukataliwa katika eneo hilo.

Katika muda wa miezi kadhaa, wimbi la chuki dhidi ya Ufaransa huko Afrika Magharibi na Kati limeshuhudia washirika wa Ufaransa waliokuwa wakiaminiwa kiuchumi na kijeshi wakiipa kisogo. Washirika hivi punde ni Senegal na Chad, ambao walivunja ushirikiano wa ulinzi na Paris wiki iliyopita.

Kuharibika huko kwa mahusiano na Ufaransa pia umeonyeshwa hadharani katika miji mikuu wa eneo hilo, ambapo umati wa waandamanaji wamepeperusha mabango yenye sauti inayojulikana sasa ya "France dégage" (Ufaransa itoke).

Nchini Niger, siku chache baada ya jeshi kuchukua mamlaka mwaka jana, umati wa watu wenye chuki walivamia ubalozi wa Ufaransa katika mji mkuu wa Niamey, na kuwataka wafanyakazi wake kuondoka nchini humo. Ilionyesha hatua ya kukata mahusiano kabisa.

Ushawishi wa ukoloni

Wataalamu wanasema kukataa kwa Ufaransa katika miongo ya hivi karibuni kuachia ushawishi wake wa kikoloni katika kile kinachojulikana kama Françafrique - neno ambalo tangu wakati huo limekuwa la dharau - hatua inayoonekana kuchangia hasira kwa kiasi kikubwa.

Kwa mfano, faranga ya CFA, sarafu inayotumiwa na nchi 14 za Afrika, bado inachapishwa nchini Ufaransa. Hadi hivi majuzi, zaidi ya wanajeshi 6,000 wa Ufaransa walikuwa wametapakaa barani Afrika huku nchi za Kiafrika zikitumai Ufaransa wangesaidia katika kupambana na makundi ya kigaidi. Hata hivyo, wanasema wanajeshi wa Ufaransa wameshindwa kuwasaidia.

Zaidi ya hayo, ushawishi mkubwa wa kiuchumi wa Ufaransa, hasa katika uchimbaji wa madini, kumesababisha lawama nyingi kwa changamoto za kiuchumi za ndani.

"Wimbi dhidi ya Ufaransa imekuwa ikiongozwa kwa njia nyingi na historia. Uhusiano huo ulianza kupungua, haswa katika muktadha wa mienendo ya nguvu isiyo sawa, ambayo ilifanya iwe ngumu kwa nchi za Kiafrika kutamani kuwa na uhuru zaidi na kujitawala kwa namna ambayo walitaka kudhibiti ajenda yao ya maendeleo na usalama," Tighisti Amare, Naibu Mkurugenzi wa Mpango wa Afrika katika Chatham House, aliiambia TRT Afrika.

Kukomesha ushirikiano

Chad wiki iliyopita iliungana na nchi nyingine za Sahel, zikiwemo Niger na Mali, katika kukomesha ushirikiano wa kiusalama na kiulinzi na mtawala wao wa zamani wa kikoloni.

Wizara ya mambo ya nje ya Chad ilisema ni wakati muafaka kwa nchi hiyo "kudai mamlaka yake kamili na kufafanua upya ushirikiano wake wa kimkakati kulingana na vipaumbele vya kitaifa."

Senegal ilifuata mkondo huo siku moja baadaye, huku Rais Bassirou Diomaye Faye akiiomba Ufaransa kufunga kambi zake za kijeshi nchini mwake.

"Senegal ni nchi huru, na uhuru haukubali uwepo wa kambi za kijeshi katika nchi huru," alisema katika ikulu yake ya rais.

Kupanuka kwa pengo la Ufaransa Afrika Magharibi na Kati na kuzibwa na mataifa mengine yenye nguvu kama Uturuki, ambayo yanafuata mkondo tofauti katika uhusiano na mataifa ya Afrika.

"Uturuki imekuwa haraka sana tangu 2009 na kuwa mshawishi muhimu barani Afrika. Mbinu ambayo imechukua imekuwa ya kuleta mwanzo mpya," alisema Amare.

"Ilianza na mbinu madhubuti ya kidiplomasia, am karibu mara nne idadi ya balozi barani Afrika, ikifuatiwa na ziara za ngazi ya juu, haswa ziara ya mwaka 2011, ambayo kimsingi iliirudisha Somalia kwenye ramani baada ya miongo kadhaa ya kutengwa kwa sababu ya ukosefu wa usalama nchini."

Faida kwa pande zote

Mbinu imekuwa kufanya maamuzi kwa kuzingatia manufaa ya pande zote katika nyanja za usalama, biashara na miundombinu.

"Nchi za Kiafrika zinatafuta nchi nyingi za kimataifa za ukubwa tofauti kufanya kazi nazo. Hazitaki kuingizwa katika uhusiano mmoja au katika mzunguko mdogo wa mahusiano. Wanatafuta kuwa na mahusiano tofauti kama njia ya kupata mambo tofauti kutoka kwa mahusiano haya" Amare alisema.

"Kwa upande wa Uturuki, kuna fursa ya kuongeza uhamishaji wa teknolojia, kwa kuzingatia nyanja ya muda mrefu ya maendeleo - ikiwa ni kuongeza uhamishaji wa teknolojia na ujuzi katika suala la kuongeza ukubwa wa tasnia yao ya utengenezaji, kama ujenzi wa viwanda, ambao ni kipaumbele muhimu kwa nchi za Afrika."

Hii Imesababisha kiasi cha biashara cha Uturuki na mataifa ya Afrika kuongezeka mara nane katika miaka ya hivi karibuni, na kuzidi pauni bilioni 40 za Uigereza, kulingana na takwimu za shirika la habari la Anadolu.

CHANZO:TRT Afrika Swahili
Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us