Na Abdulwasiu Hassan
Hapana shaka kuwa, ushawishi wa Ufaransa barani Afrika unazidi kufifia.
Uhusiano wa Ufaransa uko katika hali mbaya kwa sasa, huku baadhi ya nchi ikiwemo Senegal na Chad zikilazimika kufunga kambi za kijeshi za nchi hiyo, baada ya Niger, Mali na Burkina faso kuonesha nia ya kutoendelea na uhusiano na Ufaransa.
"Tuko kwa ajili ya Chad, Ufaransa waondoke!" walisema maelfu ya waandamanaji siku ya Disemba 6 wakiwa katika mitaa ya N'Djamena na Abeche. Wiki iliyotangulia, serikali ya Nigeria ilisema kuwa itasitisha uhusiano wake wa kijeshi na Ufaransa.
Kwa sasa, Ufaransa ni kama inatafuta afueni kwa nchi ya Nigeria.
Wachunguzi wa mambo wanasema kuwa uamuzi wa Ufaransa wa kuanzisha mahusiano na Nigeria ni mbinu ya nchi hiyo kutaka kuhuisha ushawishi wake barani Afrika.
Viongozi hao walitiliana saini mikataba mbalimbali./Picha: Serikali ya Nigeria
Mwishoni mwa mwezi Novemba, Rais Tinubu aliitembelea Ufaransa na kulakiwa na mwenyeji wake.
Macron pia aliwahi kufanya kazi katika ubalozi wa Ufaransa nchini mjini Lafos mwaka 2002, wakati Bola Tinubu akiwa ni gavana wa eneo hilo.
Hata hivyo, uenyeji aliopewa Tinubu pamoja na mikataba waliyosainia na Macron inaashiria azma ya Macron kurudisha mahusiano hayo.
Hata hivyo, hatua hiyo imeibua gumzo kubwa nchini Nigeria.
Kulingana na Dkt Aminu Hayatu, mtafiti wa sayansi ya siasa kutoka Chuo Kikuu cha Bayero mjini Kano, uamuzi huo ni wa kimtego kwa taifa hilo kubwa la Afrika Magharibi.
Tayari, nchi za Niger, Mali na Burkina Faso zimetengeneza umoja wa kupambana na ugaidi./Picha: Reuters
"Ufaransa ipo katika wakati mgumu kwa sasa, sio Ufaransa tu, hata mataifa mengine makubwa ya magharibi," anaiambia TRT Afrika.
"Wakati Nigeria ikitafuta fursa ya kiteknolojia ya Ufaransa, si vyema kudharau matamanio yake kwa Nigeria," anaonya.
Mkataba wa maelewano uliotiwa saini kando ya ziara ya Rais Tinubu unataja kwamba nchi hizo mbili "zitashirikiana katika utafiti, mafunzo na kubadilishana wanafunzi wa Kifaransa na Nigeria kwa ajili ya ujuzi na uhamisho wa ujuzi". Mkataba huo pia unahusisha ushirikiano katika kutumia rasilimali za madini za Nigeria.
Wanigeria wanaofahamu mateso ya kikoloni ya zamani na ushawishi mkubwa wa baada ya ukoloni wa Ufaransa katika sehemu fulani za Afrika wanahofia makubaliano yoyote na mamlaka ya Ulaya.
Mara tu baada ya kutangazwa kwa mpango huo, Wanigeria wengi walionesha kukerwa na hofu juu ya uwezekano wa kunyakuliwa kwa sekta ya madini ya nchi hiyo na Ufaransa, kama ilivyokuwa katika nchi nyingine kadhaa katika eneo hilo.
Serikali ya Nigeria ililazimika kutoa tamko kujaribu kupunguza hatari zinazohofiwa. "Wafaransa hawachukui sekta ya madini ya Nigeria," Mshauri Maalumu, Vyombo vya Habari na Mawasiliano ya Umma kwa Rais Tinubu, Sunday Dare, alisema katika taarifa hiyo.
Hisia kubwa miongoni mwa raia wa Mali, Burkina Faso na Niger ni kwamba kuendelea kuwepo kwa Ufaransa, hata baada ya uhuru, kuliongeza changamoto zao za usalama badala ya kuwarahisishia.
"Mahusiano yote yana historia na vigezo tofauti. Uhusiano wa nchi hizi (Mali, Burkina Faso na Niger) walikuwa nao na Ufaransa ni tofauti kabisa na wa Nigeria," Abdulaziz Abdulaziz, msaidizi mwandamizi maalum wa Rais Tinubu, anaiambia TRT Afrika.
"Kwamba majirani hawa wana matatizo na Ufaransa haitoshi sababu ya sisi kuwa na tatizo nayo. Haifanyi kazi hivyo," anaeleza.
Baadhi ya wachambuzi wanasema Nigeria haipaswi kuchukulia uhusiano wake na Ufaransa kwa thamani ya usoni, na kwamba uhusiano huo ni lazima kuwa na athari mbaya zaidi ya nchi hiyo.
"Ikiwa mataifa mengine katika kanda yanaona kuongezeka kwa ukaribu wa Nigeria na Ufaransa kama tishio kwao, inaweza kusababisha kuongezeka kwa mvutano na ushindani ndani ya kanda," anasema Dkt Hayatu.
Wachambuzi pia wanaamini kuwa licha ya Ufaransa kuweka matumaini kwa Nigeria, kuongezeka kwa chuki dhidi ya Ufaransa na wimbi la harakati za Waafrika katika eneo hilo kunamaanisha kuwa eneo hilo linabaki kuwa gumu kwa mkoloni huyo wa zamani.