Jumuiya ya Mamlaka ya Kimataifa kuhusu Maendeleo (IGAD) imepongeza makubaliano ya kihistoria kati ya Somalia na Ethiopia ambayo yamemaliza takriban mwaka mmoja wa mvutano, kufuatia mazungumzo katika mji mkuu wa Uturuki.
Workneh Gebeyehu, katibu mtendaji wa Mamlaka ya Maendeleo ya Kimataifa (IGAD), alitoa shukrani zake kwa Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kwa jukumu lake kubwa katika kuandaa na kuwezesha mijadala iliyozalisha Azimio la Ankara siku ya Jumatano 11, Disemba 2024.
"Makubaliano haya muhimu yanaashiria hatua kubwa ya kuimarisha mfumo wa kijamii wa muda mrefu kati ya mataifa hayo mawili yenye undugu na kuonyesha dhamira ya kusuluhisha masuala ya pande mbili kwa amani," Gebeyehu alisema katika taarifa yake siku ya Alhamisi.
Akitambua kujitolea kwa Erdogan kwa diplomasia na ushirikiano wa kikanda kama jambo muhimu katika kufikiwa kwa makubaliano hayo, Gebeyehu alisisitiza umuhimu wa "juhudi kama hizo za kidiplomasia katika kushughulikia changamoto za pamoja na kukuza utulivu na ustawi katika Pembe ya Afrika."
Juhudi za kumaliza mivutano
Nchi hizo mbili za Afrika Mashariki zimekuwa katika mzozo tangu Ethiopia ilipofikia makubaliano na eneo lililojitenga la Somalia la Somaliland mnamo Januari 1 kutumia bandari yake ya Bahari Nyekundu ya Berbera. Uturuki imekuwa ikifanya kazi ya kumaliza mvutano kati ya nchi hizo mbili.
Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, na Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamoud walifanya mkutano na waandishi wa habari katika mji mkuu wa Uturuki Ankara wakitangaza makubaliano yaliyofikiwa wakati wa mazungumzo ya amani yaliwezeshwa na Uturuki.
Katika azimio hilo la pamoja, mataifa hayo mawili ya Kiafrika yalithibitisha uhuru wa kila mmoja wao, umoja na uhuru, na kuahidi kuanzisha mazungumzo ya kiufundi na yakisimiwa na Uturuki mwishoni mwa Februari 2025 na kuhitimisha ndani ya miezi minne.
Mnamo 1991, Eritrea ilipata uhuru kutoka kwa Ethiopia, na kusababisha kuanzishwa kwa mataifa mawili tofauti. Utengano huo ulisababisha Ethiopia kupoteza ufikiaji wa moja kwa moja kwenye Bahari Nyekundu na bandari kuu.