Uturuki inatarajia kuuona Umoja wa Ulaya ukichukua hatua stahiki za kuboresha mahusiano, Rais wa Uturuko Recep Tayyip Erdogan amemueleza Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Antonio Costa.
Akimpongeza Costa kufuatia uteuzi wake ndani ya baraza hilo, kwa njia ya simu siku ya Alhamisi, Erdogan alisema kuwa kuhuisha uhusiano kati ya Ankara na Brussels ni jambo la manufaa kwa pande zote, kulingana na taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Uturuki kwenye ukurasa wa X.
Erdogan na Costa pia walijadiliana masuala ya kikanda, kiulimwengu, huku Rais wa Uturuki akisisitizia kuwa itakuwa ni muhimu kwa maslahi ya pande zote mbili.
Kulingana na kiongozi huyo wa Uturuki, suala la upatikanaji amani kati ya Urusi na Ukraine ni jambo linalowezekana, kwani Ankara imekuwa ikifanya jitihada ya upatikanaji amani toka kuanza kwa vita hivyo.
Pia, alionesha kuridhishwa na hatua ya Umoja wa Ulaya ya kuiondolea vikwazo Syria.
Costa alimtakia heri Erdogan katika kumbukizi yake ya kuzaliwa, wakati wa mazungumzo hayo.
Hapo awali, Umoja wa Ulaya ulitangaza kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Syria, haswa kwenye sekta za nishati, usafirishaji na sekta ya kifedha ili kuisaidia ujenzi mpya wa nchi hiyo.