Afrika
2 dk kusoma
WHO inasema Mpox bado ni ugonjwa wa dharura
Nchi 22 barani zimeathiriwa na virusi vya Mpox huku 14 zikiwa katika hatua ya mlipuko na zingine nane katika hatua ya udhibiti.
WHO inasema Mpox bado ni ugonjwa wa dharura
Kamati ya Dharura ya WHO imeamua mpox kama bado ni ugonjwa wa dharura duniani
tokea masaa 6

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO Dkt. Tedros Adhanom Ghebreyesus alitangaza kwamba kuongezeka kwa maambukizi ya Mpox kunafanya ugonjwa kuwa na sifa za dharura kwa afya ya umma, kama ilivyoainishwa katika Kanuni za Afya za Kimataifa.

Tangazo hilo linafuatia mkutano wa tatu wa Kamati ya Dharura ya WHO kuhusu kuongezeka kwa Mpox.

Kamati ilimshauri Mkurugenzi Mkuu kusisitiza kuhusu hali ya dharura ya ugonjwa huo kimataifa, kulingana na kuongezeka kwa idadi ya watu walioambukizwa, na ghasia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wataalamu wa afya wanasema mzozo DRC unafanya iwe vigumu kuwafikia watu walioambukizwa Mpox maeneo mbalimbali na kuwapa matibabu.

Mpox barani Afrika

Mlipuko wa Mpox kimataifa ulianza Mei 2022 na unaendelea hadi leo.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari 27 Februari 2025 shirika la afya barani, Afrika CDC lilisema tangu nwanzo wa Januari 2025 maambukizi ya Mpox barani yamefika 21,544 katika nchi tofauti.

Kati ya maambukizi hayo, 5,364 yamethibitishwa kuwa ugonjwa huo .

Nchi 22 barani zimeathiriwa ikiwa 14 zipo katika hatua ya mlipuko na zingine nane katika hatua ya udhibiti.

Kumekuwa na vifo vya watu 233 ambavyo vimeripotiwa kwa walioshukiwa kuwa na ugonjwa huo na vifo 13 waliothibitishwa kuwa na maambukizi hayo.

Afrika CDC pia imesema Afrika Kusini imethibitisha maambukizi matatu mapya baada ya kutokuwepo kwa maambukizi kwa siku 90.

Sudan Kusini na Congo Brazaville pia zimeripoti maambukizi mapya.

Hali nchini DRC

Afrika CDC inasema kuna aina mpya ya virusi vya Mpox nchini DRC ambavyo vinasemakana kuwa na uwezo wa kusambaa haraka.

“Kwa sasa DRC imeanza kutoa chanjo dhidi ya Mpox kwa maeneo hasa ya Kinshasa na hii inaonesha jamii inaelewa na kukubali kujikinga dhidi ya hatari hii,” anasema Dkt. Ngashi Ngongo, mtaalamu wa Mpox katika shirika la Afrika CDC.

DRC inalenga kutao chanjo kwa zadii ya watu 600,000.

Mlipuko wa ugonjwa unaenea kwa kiasi kikubwa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Burundi na Uganda, huku maambukizi mapya yanayotokana na watu kusafiri yakibainika katika nchi ambazo hazikuwa na maambukizi hapo awali.

“Licha ya maeneo mengi nchini DRC kuripoti mienendo thabiti ya maambukizi, hali nchini inabaki kuwa ya wasiwasi, huku maeneo mengi yakiwa na maambukizi yanayoenea. Kuongezeka kwa vurugu katika eneo la mashariki mwa nchi kunaleta changamoto zaidi kufikia maeneo yaaliyoathiriwa na Mpox,” WHO imesema katika tahmini yake ya Februari 2025.

Tazama TRT Global. Shiriki maoni yako!
Contact us